
Uongozi wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba ramba. Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite. Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni